Thursday, May 1, 2025

Mwanaume – Fahamu Haya Ili Uwe Bora Katika Mahusiano

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


 Mwanaume – Fahamu Haya Ili Uwe Bora Katika Mahusiano

 

Mwanamume anayeweza kudhibiti hamu ya tendo ni mtu anayeweza kuishi miaka mingi duniani. Wanaume hawajui kwamba baadhi ya kushindwa kudhibiti hamu husababishwa na kuwa na wanawake wengi japo Sio wanaume wote.


Wanawake wengine wanakuja kwako kwa lengo la uharibifu.
kuwa Makini sana:

1. Mwanaume wa kweli ana mwanamke mmoja tu maishani mwake.

2. Usiruhusu kupandisha hisia wakati wote. Mishipa mingi huchoka kudhibiti uume wako ikiwa hutaki kudhibiti hali hiyo.

3. Usimchumbie mwanamke kwa sababu ana umbo zuri, matiti na umbo la kuvutia. Haya mambo ni ya kupotosha.

4. Sio kila unachokiona chini ya sketi lazima ukifanyie kazi. kudhibiti hamu zako za ngono au Kujidhibiti na kujiepusha kuna faida sana

5. Kuoa mwanamke maana yake unammiliki lakini Mtendee mema kwa heshima Mfanye kuwa malkia wako, mpende, mheshimu na mpe sababu za kukutendea sawa.

6. Kuwa na mahusiano ya wanawake wengi hakukufanyi kuwa mwanaume bora. Inakufanya tu kuwa mwanaume, mdanganyifu na kukutoa ukubwani na kurudi kuwa mvulana.

7. Kwa sababu wewe ni mzuri kitandani hakukufanyi kuwa mwanaumebora. Mwanaume wa kweli ni mwanaume yule asiyekimbia wajibu na majukumu yake na kuamua kukabiliana nayo
.
8. Mheshimu mwanamke yeyote anayekupenda, si rahisi kwa mwanamke kutupa upendo wake na kusaidia kwenye maisha yako ikiwa unaishi kwa kumuumiza tu.

9. Leo hii Dunia inasherehekea wanaume waliofanikiwa Hakuna atakayekusherehekea kuwa na wapenzi wengi wa kike. kitendo hiki ni sawa na Upotevu wa nishati, pesa na upotevu wa mbegu za kiume.

Kumbuka, kuwa mwaminifu akikutana na mwaminifu ni alama ya ushindi katika ndoa

Add Comments


EmoticonEmoticon