Friday, May 2, 2025

Mwanaume Elewa haya Mambo - Hautanyanyaswa na Mwanamke katika Mahusiano

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


NJIA 7 AMBAZO MWANAUME RIJALI ANAWEZA KUYASHINDA MAUDHI, MAJARIBU NA VITIMBI VYA MWANAMKE KATIKA MAHUSIANO


Tafiti za kisaikolojia zinaeleza kwamba wanawake hawajui wanataka nini kutoka kwa mwanaume hivyo basi ikiwa wewe ni mwanaume acha kupoteza muda wa kutaka kujua mwanamke anataka nini bali weka sheria na muongozo wako mwenyewe kisha mwanamke wako ataufuata.

ZIFUATAZO NI NJIA 7 AMBAZO MWANAUME RIJALI ANAWEZA KUYASHINDA MAUDHI, MAJARIBU NA VITIMBI VYA MWANAMKE KATIKA MAHUSIANO


Njia hizi 7 zipo kama ifuatavyo


1. KUPIMA UANAUME WA MWANAUME (DOMINANCE TEST)
Mwanamke yeyote ambaye nyumbani kwao mkuu wa familia ni mama,au amekuwa bila baba ndani ya familia,au baba yake mzazi alikuwa dikteta,au baba yake mzazi ni mpole kupitiliza kiasi kwamba hana kauli wala mamlaka yoyote ndani ya familia huwa anapenda kumfanyia mwanaume jaribio hili.

Mwanamke hapa anataka kuwa kichwa cha familia hivyo ataonyesha tabia zifuatazo -atampangia mwanaume sheria,atampa mwanaume maagizo,atamfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza, kumtangaza vibaya,kumtishia kumuacha mara kwa mara,atamwabia mwanaume chagua mimi au mama yako mzazi,

atampiga marufuku mwanaume wake mara kwa mara kwa kumchagulia marafiki,kumpangia matumizi ya fedha, kumpangia muda wa kurudi nyumbani, kumuamrisha mwanaume atoe fedha nyingi sana ikiwemo kukabidhi mshahara wake wote kisha Mwanamke anapanga matumizi.

Atamkosoa mwanaume mara kwa mara kwanzia muonekano, uvaaji, utembeaji, lafudhi,harufu ya mwili, usafi wa mwili,atakuwa anamrekebisha mwanaume wake tabia kila siku,atamnyima unyumba mwanaume wake kwa makusudi kama adhabu,

Atamwabia mwanaume siwezi kupangiwa cha kufanya,atakuwa haambiwi makosa,atakuwa hashauriki, haambiliki, anakuwa mjuaji sana, anakuwa na hasira kupitiliza, anakuwa na misimamo mikali sana ( rigid),akiamua jambo lolote ni hivyo hivyo hawezi kubadili mawazo,anakuwa anataka kuwa juu saa 24,hataki kukosolewa, hataki kuambiwa makosa yake, hataki,kupewa maagizo.

UFUMBUZI WAKE
Huyu mwanamke ni maalumu kwa ajili ya kuzaa kila mtoto na baba yake kisha huwa anatelekezwa bila huduma zozote, vilevile mwanamke huyu huwa maalumu kwa ajili ya kuzaa na waume za watu.
Hawezi kukubali kuongozwa ndani ya familia kwa sababu tangu utotoni anaamini ni UTUMWA kuwa chini ya mamlaka ya mwanaume.

ufumbuzi wake ni kumrudisha nyumbani kwao akae mpaka akili ikimkaa sawa,atakubali kuwa mwanamke.Hili ni zao la feminist.

2. KUPIMA UWEZO WA MWANAUME KUJIAMINI (CONFIDENCE TEST)
Ili mwanamke aruhusu mwanaume kumuongoza lazima mwanaume aonyeshe uwezo wa kujiamini mbele ya mwanamke husika.
Ikiwa mwanaume hajiamini vilevile mwanamke atampuuza,mwanaume hawezi kumuongoza mwanamke ikiwa yeye mwenyewe hawezi kujiongoza.

Mwanamke akiona mwanaume ananyenyekea sana,anaomba msamaha mara kwa mara,anapiga magoti,anatuma sms ndefu sana,anajishusha sana huanza kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza,kumjibu vibaya,kusema wewe sio wa HADHI yangu .

Ufumbuzi wake ikiwa wewe ni mwanaume epuka tabia za upole, huruma kupitiliza, kujali sana, kunyenyekea sana, kusamehe makosa haraka badala yake simama kama kiongozi shupavu, mwambie ninakuheshimu sana fulani, sihitaji tuvunjiane heshima,akiwa na heshima mwanamke huyo ongea naye kwa utulivu,tazama usoni,zungumza kwa pause,usiongee haraka haraka sana au polepole sana,epuka kuonyesha hasira pale ambapo mwanamke anapoonyesha dharau mbele yako.

3. KUPIMA WIVU WA MWANAUME (JEALOUS TEST)
Mwanamke anaweza kupima wivu wa mwanaume kwa kupuuza sms,kupuuza simu,kupost picha za wanaume wengine, kuzungumza habari za Ex wake,anaweza kusema kuna mwanaume anamtongoza, anaweza kuzungumza na mwanaume mwenzako mbele yako kwa kujilegeza legeza, anaweza kuchat mpaka usiku wa manane lengo uone wivu,au anaweza kukaa na simu muda wote.
Hapa epuka kupaniki,epuka kuonyesha hasira,epuka kuonyesha kwamba hauwezi kuishi bila yeye.

Ongea kwa utulivu kwamba ûnampenda sana na unamuheshimu lakini ikiwa atashindwa kukuheshimu na kukuacha uwe mwanaume kamili katika maisha yake utamuacha uende sehemu ambayo unapewa heshima..

Hapa nguzo ni mwanaume kuonyesha UONGOZI wake mahiri.

4. KUPIMA KAMA MWANAUME ANAWEZA KUMPA CHANGAMOTO (CHALLENGE TEST)
Wanawake ambao ni "wife material" hawavutiwi kimapenzi na wanaume wenye tabia za huruma kupitiliza, kujali sana, kunyenyekea sana, kusamehe makosa haraka, uvumilivu uliopitiliza, wastaarabu sana,bwana ndiyo,mwanaume mpenda amani,mwanaume ambaye anajishusha sana.
Ukiwa na sifa hizo unapata mwenza mwenye tabia ya ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri, ujuaji, misimamo mikali,anakuwa anataka kumtawala mwanaume,anataka kila mtu na kila kitu kiwe chini yake, mwanamke ambaye anataka uhuru uliopitiliza huwa anavutiwa kimapenzi na mwanaume mpole kupitiliza kwa sababu anakuwa anataka kumtawala, kumpangia sheria,kum-control, kumgombeza, kumbambikia ujauzito n.k

Mwanamke ambaye ni wife material akiona mwanaume anatabirika,mwanaume ni mstaarabu sana anaanza kumchukia kwa sababu anahisi anaishi na mwanamke mwenzake.
Kuwa mwanaume ambaye hautabiriki,zipo nyakati unakuwa mpole kiasi vilevile zipo nyakati unakuwa mkali kiasi.Lengo mwanamke asijenge kiburi cha kuamini kwamba hauwezi kuishi bila yeye,hauwezi kumuacha hata afanye kosa kubwa namna gani.

Zingatia kwamba mwanamke yeyote akiwa na uhakika kwamba ûnampenda sana kuliko kitu chochote hapo ndipo anakuwa na kiburi, majivuno, jeuri, ujuaji, misimamo mikali,anakuwa na masharti magumu sana, anaweza kufanya makosa makubwa sana kwa makusudi kabisa kisha anageuza kibao kwako.
Hot & cold response

5. KUTAFUTA KISINGIZIO CHA KUACHANA (NUCLEAR TEST)
Mwanamke anapotaka muachane huonyesha tabia zifuatazo
atakaa kimya muda mrefu sana,simu hapokei, ukituma sms hajibu, au ukitumia namba mpya anapokea kisha anatafuta kisingizio cha kukata simu.

ataomba fedha nyingi sana kuliko uwezo wako lengo ukishindwa tu anakuacha,atakuwa na kiburi, majivuno, jeuri na dharau katika kuzungumza na wewe.
Anaweza kukudhalilisha mara kwa mara,anakulinganisha na wanaume wengine kisha anasema wewe sio wa HADHI yake,mara kwa mara anakuwa na hasira kupitiliza akiona sura yako.
Utajikuta unafanya kazi kubwa sana kumfurahisha lakini anakuwa hana huruma wala hana shukurani kwako.
Mara kwa mara atakuwa anakukosoa kwa vitu vidogo vidogo sana ili muachane kwa ugomvi.
Akionyesha tabia hizo haitaji ushauri,haitaji kubembelezwa,hataki risala,hataki kuambiwa makosa yake, hataki umlazimishe aseme hatma ya mahusiano yenu,hataki umkumbushe wema wako kwake,hataki kusikia maisha yake yatakuwa magumu bila wewe.Hapo anataka muachane tu.

6. KUKAA KIMYA BILA MAWASILIANO KWA MAKUSUDI (UNEXPLAINED DISTANCE)
Wanawake wenye tabia za ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri na dharau hupenda sana tabia hii (ghosting).Yaani leo mnaongea kwa furaha sana kisha kesho simu hapokei, ukituma sms hajibu.
Ukipiga simu kwa namba mpya anapokea kisha akisikia sauti yako anakata.
Hapa anataka kukuvuruga akili uanze kujiuliza wapi umefanya makosa lakini haupati jibu.
Endapo utapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo, kulalamika kwamba hauna furaha kwa ukimya wake anapata kiburi cha kuamini kwamba hauwezi kuishi bila yeye, hauwezi kumuacha hata afanye kosa kubwa sana namna gani.
Tabia hii anakuwa anataka kujua kama umeshampenda sana akiona unaonyesha kubabaika kwa ukimya wake dharau, majivuno,na kukutesa huwa ndiyo tabia zake.

Ufumbuzi wake -Akikaa kimya sana bila mawasiliano yoyote,acha kupiga simu,acha kutuma sms, ilimradi umepiga simu hajapokea na umetuma sms hajajibu.
Kaa kimya muonyeshe kwamba yeye ni binadamu kama walivyo binadamu wengine wala hauwezi kuteseka kwa ukimya wake vilevile kama ataamua muachane pengo lake unaziba na unamtoa kichwani haraka.

7. KUVUNJA MAKUBALIANO GHAFLA (FLAKE TEST)
Njia nyingine mwanamke anatumia ni kuvunja makubaliano ghafla.
Hapa inatokea umekubaliana na mwenza wako tunakwenda sehemu XYZ,muda ABC kisha baada ya makubaliano anasubiri nusu saa kabla ya muda wa tuko lenyewe anatuma sms kwamba amepata dharura au anakaa kimya tu bila sababu zozote za msingi (ghosting).

nini cha kufanya zingatia sababu za hali hiyo
a.Hana hisia zozote kwako lakini anashindwa kukataa
b.Anakujaribu ili kupima tabia yako ikoje
c.Ipo sababu ya msingi ambayo ni DHARURA kwa muda huo.

ufumbuzi wake acha kupiga simu mfululizo,acha kutuma sms mfululizo.
kaa kimya muonyeshe kwamba yeye kukaa kimya haijaleta athari zozote katika ratiba yako.
Endapo utapiga simu mfululizo na kutuma sms mfululizo itamfanya aweze kuwa na kiburi, majivuno, jeuri,dharau na vilevile anakuona haujielewi kwa maana anaona hauwezi kuishi bila yeye, hauwezi kumuacha na vilevile furaha yako anaicontrol yeye.

Kaa kimya,muache apange ratiba nyingine yeye mwenyewe,kama alikuwa anakupima atakuja na visingizio kibao,kama alikuwa anataka muachane utakuwa umeokoa fedha zako na muda wako ambao ungepotea kwa mtu huyo.

Add Comments


EmoticonEmoticon