Thursday, May 1, 2025

Mwanamke anapokwambia Tuachane isiyomaanisha, akiwa kwenye Muonekano unaoitwa Seriously - Jifunze Kitu hapa

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


Mwanamke anaweza kukwambia tuachane isiyomaanisha, akiwa kwenye mwonekano unaoitwa seriously.


Kisha akabadilika kuwa kwenye huzuni ya kweli, kama utaamua kukubaliana na yeye.

Kwasababu alihitaji umbembeleze, sio utembelee kauli yake.

Ngoja nikwambie kitu mwanaume mwenzangu.

Siku mojamoja kuwa Kaisal kimaandishi, halafu msomee kwa sauti ya Khan Mbarouk.

Mwambie licha ya udhaifu wako wa kutamani wengi, lakini unampenda peke yake.

Msimulie hadithi za kina Sharifa na Sarah, walioahidi kukupa hadi Mungu alivyovikataza.

Mwambie amestahili kuwa na wewe, sio bahati kama mitaa inavyozungumza.

Mkumbushe sifa ulizomwongopea, kipindi cha harakati zako za kumtongoza.

Mwambie unamwona malaika aliyetoroka peponi, kila unapomtazama Eva wako wa Vikindu.

Mfanye ajione special sana kwenye hii dunia, mwambie hauna maisha yanayoeleweka, kama ataamua kuishi mbali na wewe.

Wakati mwingine tunawapoteza wa ndoto zetu, kwa kufeli course nyepesi ya kuelewa hisia zao tu.

Mpe kitu cha kujivunia ndani ya moyo wake, tofauti na tukio la kumheshimisha ngariba wako.

Mwanamke ni kama uyoga, sumu yeye, chakula yeye, wako jitahidi umwelewe.

Add Comments


EmoticonEmoticon