Saturday, May 3, 2025

Madhara ya Kuwapenda WASIOKUPENDA na Kuwachukia Wanaokupenda

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


 LIMERENCE:

TATIZO LA KUWAPENDA SANA WATU AMBAO HAWAKUTAKI NA KUWACHUKIA SANA WATU AMBAO WANAKUPENDA SANA


LIMERENCE ni neno la kiingereza lenye maana ya hali isiyoweza kuzuilika ya kiakili na kihisia ambayo husababishwa na hisia za mapenzi kwa mtu mwingine ambapo mtu hujikuta anatumia muda mrefu sana kumfikiria sana mwanaume au mwanamke huku akitamani mtu huyo aonyeshe kiwango kilekile cha upendo ambacho yeye anakuwa nacho kwa mtu huyo.

Kwa maana kwamba unamuona mwanaume au mwanamke popote pale kisha unakuwa na hisia kali sana za mapenzi juu yake mpaka unaanza kujenga taswira ukiwa na mtu huyo kitandani au ukiwa umemuoa au umeolewa naye.Lakini mtu huyo anakuwa hajui chochote.

Vilevile hata pale ambapo unakuwa umejenga naye mahusiano unajikuta unakuwa na hisia kali sana za mapenzi juu yake kiasi kwamba unakuwa na hofu ya kuachwa muda wote.

kwa leo tuangalie viashiria vya tatizo la kisaikolojia la LIMERENCE,kisha tuangalie athari za LIMERENCE namna husababisha mtu kuumizwa sana kwenye mahusiano.

VIASHIRIA VYA TATIZO LA LIMERENCE
Mtu yeyote ambaye anasumbuliwa na tatizo la kisaikolojia la LIMERENCE huwa anaonyesha viashiria vifuatavyo

-Unakuwa na hisia kali sana za mapenzi kwake kuliko kwa mtu yeyote
- Unatumia muda mrefu sana kumfikiria sana mtu huyo,mara kwa mara unakuwa unafikiria namna utamuokoa endapo atakuwa kwenye matatizo
-Unakuwa unatafuta kiashiria chochote kama anakupenda mfano akionyesha tabasamu au akicheka unahisi anakupenda sana

-Unapata utulivu mkubwa sana kwake ukiwa naye karibu kuliko ukiwa na mtu yeyote
-Kama ukimuona anazungumza na mtu mwengine unapata wivu mkali sana na unaweza kuingilia mazungumzo yao

-Unatafuta mazingira kwa nguvu zote ili upate kuonana naye au kuwasiliana naye.
-Unaona mazuri yake tu na kupuuza mabaya yake na mapungufu yake,mazuri yake unaona ni makubwa sana kuliko mtu yeyote na makosa yake unayapuuza kuliko makosa ya watu wengine,unavumilia tabia zake zenye maudhi ambazo awali ulikuwa hauwezi kuvumilia kutoka kwa watu wengine.

-Unakuwa na wasiwasi muda wote,kama hakuna mawasiliano baina yenu unahisi tayari amekuacha na amekwenda kumpenda mtu mwingine,endapo akikaa kimya bila mawasiliano.

-Unaamini hauwezi kuishi bila yeye, hali hii inaweza kukufanya ujitoe mhanga kwake ili akuone mtu muhimu sana kwenye maisha yake ili iwe rahisi kukupenda kama vile ambavyo ûnampenda,unataka uwe naye karibu muda wote,ukiwa mbali naye unakosa furaha.

-Unafanya juhudi kubwa sana ili muwe pamoja lakini yeye hafanyi juhudi zozote ili muwe pamoja

ATHARI ZA LIMERENCE
LIMERENCE inaweza kusababisha athari zifuatazo katika mahusiano

1. KUTAKA KUMBADILISHA TABIA ILI AJE KUWA MWENZA WA NDOTO ZAKO
a.Mwanamke hugeuka mama mzazi kwa mwenza wake
Mwanamke mwenye kusumbuliwa na LIMERENCE hufanya mambo yafuatayo
-Anavutiwa kimapenzi na mwanaume ambaye hana kazi yoyote wala hataki kufanya kazi,hapo Mwanamke huamua kumtafutia kazi lakini anakataa,atampa mtaji kisha mwanaume anakula,atamchukulia mkopo lakini mwanaume anakwenda kulewa na kuhonga pesa inakwisha anarudi nyumbani kukaa sebuleni akitazama Tv

-Mwanamke atahudumia watoto,atajenga kwa pesa zake, lakini mwanaume yupo tu nyumbani hana MSAADA wowote lakini Mwanamke anakuwa hana ujasiri wa kumuacha mwanaume huyo

-Mwanamke atafanya kazi ya kumbadilisha tabia mwanaume kama vile kuacha pombe,kuacha wizi,kuacha uvutaji bangi,kuacha uhalifu lakini mwanaume anakuwa hivyo hivyo miaka yote na mwanamke anakosa ujasiri wa kumuacha mwanaume huyo.

-Mwanaume kazi yake ni kumpiga, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza, kumtangaza vibaya, kumlaumu, kumdhalilisha, kumuingilia kinguvu wakati huohuo mwanaume huyo anaishi kwa kutegemea fedha za Mwanamke.

b.Nice guy
hapa ni eneo la mwanaume, LIMERENCE husababisha mwanaume anavutiwa kimapenzi na Mwanamke mwenye hulka ya kiume (Masculine woman) - mwanamke anakuwa na tabia za ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri, ujuaji, misimamo mikali sana, mwanamke anakuwa hashauriki, haambiliki, anakuwa hataki kuambiwa makosa yake, hataki kuambiwa cha kufanya,anakuwa na lugha ya udhalilishaji,

mwanaume anakuwa anapangiwa sheria,anapelekeshwa , anagombezwa lakini mwanaume anakuwa hana sauti yoyote ya kujitetea.

2. KUWEKEZA FEDHA NYINGI SANA ILI KUBORESHA MAISHA YAKE LAKINI ANAKUGEUKA BAADAYE
Hapa mwanaume ambaye anasumbuliwa na tatizo la kisaikolojia la LIMERENCE huwa anafanya uwekezaji mkubwa sana kwa mwanamke kama ifuatavyo
-Atakutana na mwanamke ambaye ameumizwa kwenye mahusiano labda amemtendwa au ametelekezwa na ujauzito au watoto kisha mwanaume anafanya kazi ya kumfariji, kumlinda, kumliwaza, kumtetea lakini Mwanamke anakuwa hana huruma,hana shukurani,anakuwa na masharti magumu sana na misimamo mikali sana,anampangia mwanaume sheria kisha mwanaume anakubali

baada ya hapo mwanaume anafanya uwekezaji mkubwa sana kama vile kumsomesha, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama kubwa sana,kumjengea nyumba, kusomesha watoto ambao Mwanamke alitelekezwa nao

lakini katika hali ya kustaajabisha mwanamke huyohuyo baada ya kuanza kupendeza,kusimama vizuri kiuchumi anarudiana na mzazi mwenzie (Ex wake) kisha anamuacha Nice guy bila kumuonea huruma hata chembe kisha akifika kwa mzazi mwenzie anakabidhi fedha zote na mali zako alizopewa na huyu Nice guy kisha baada ya muda anapewa ujauzito kisha anafukuzwa kwa mara ya pili, kisha Mwanamke huyohuyo anarudi kuomba msamaha kwa yule Nice guy aliejitoa mhanga kumfariji na kubadilisha maisha yake mara ya kwanza .

3. KUVUMILIA MATESO NA MANYANYASO KWENYE MAHUSIANO
madhara ya LIMERENCE ni uvumilivu uliopitiliza wa manyanyaso na mateso kwenye mahusiano.
mwanamke anaweza kuvumilia unyanyasaji wa kimwili kama vile vipigo
-Vipigo hapa kunahusisha -kubamizwa ukutani,kupigwa vibao usoni,kuvutwa nywele, kuburuzwa sakafuni,kuchomwa moto,kuchomwa pasi ya umeme,kubanwa na plaizi,kupigwa mateke,kulazwa kwenye miiba,kufungiwa ndani, kufukuzwa nyumbani usiku wa manane,kukojolewa mwilini,kukabwa kooni,kutishiwa kuuawa.

-Manyanyaso ya kihisia anaweza kufanyiwa yeyote
ambapo kunakuwa na mfululizo wa kauli zenye kuumiza kama vile ,-kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kufanywa kichekesho, kugombezwa, kukaripiwa, kupelekeshwa,kutukanwa wazazi wako, kumshambulia kwa maneno makali sana,

kuitwa majina ya udhalilishaji kama vile "mbwa",au kuambiwa "Hauna akili",
"Unanuka sehemu za siri usinisogelee"
"wewe ni laana"
"wewe ni mkosi"
"Hauna hadhi ya kuwa na mimi"
"Mimi nikikuacha haupati mtu kama mimi"

Add Comments


EmoticonEmoticon