Friday, May 2, 2025

Baada ya Mahusiano yako Kuvunjika - Jifunze haya Mambo upone Kihisia

 Jiunge na Magroup yetu

TELEGRAM | FACEBOOK


Mambo 5 Ambayo Utajifunza Baada Ya Mahusiano Kuvunjika


Kila mtu huwa anajifunza kitu tofauti katika mazingira tofauti.Ikitokea mahusiano kuvunjika wapo hujifunza kuacha kuamini jinsia tofauti maisha yao yote , vilevile wapo huamua kujifunza kujichukia wao wenyewe, vilevile wapo hujifunza kwenye makosa yao lakini vilevile wapo ambao hawaamini kama wanakosea popote.

Kwa vyovyote itakavyokuwa mahusiano kuvunjika huacha athari hasi au chanya, mahusiano kuvunjika yanaweza kukusaidia au kukuharibia.

tuangalie mambo 5 ambayo unaweza kujifunza baada ya mahusiano kuvunjika
MAMBO 5 AMBAYO UTAJIFUNZA BAADA YA MAHUSIANO KUVUNJIKA
Mambo hayo 5 kwanzia namba moja mpaka namba tano.

1. MAUMIVU YA MAPENZI NA AIBU YA MAHUSIANO KUVUNJIKA
Baada ya mahusiano kuvunjika kila mtu huwa na njia zake za kukabiliana na maumivu ya mapenzi,wapo hujifunza kuboresha tabia zao ili waweze kufurahia mapenzi siku za baadaye,wengine hujifunza kuwa na mioyo migumu sana na kuacha kuruhusu mtu yeyote kuingia maishani mwao.

Aibu na fedheha ya kuachwa ghafla na mwenza husababisha tabia zifuatazo kwa watu
a.Kumshambulia kwa maneno makali sana Ex wake ,pamoja na kumdhalilisha sana kwa kauli kama "mtu mwenyewe alikuwa choka mbaya,alikuwa lofa masikini wa kutupwa,mtu mwenyewe hana sura wala shape,mtu mwenyewe hakuwa na hadhi ya kuwa na mimi basi tu nilimsitiri asidhalilike"
watu wenye tabia ya ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri na dharau pale ambapo wameachwa huongea maneno hayo kwa sababu wao hujiona ndiyo wanatakiwa kuacha wenzao na maumivu makali sana miaka yote,wao kuachwa huona aibu na fedheha kupitiliza.

b.Kujishambulia na kujidhalilisha yeye mwenyewe kwa maneno makali sana baada ya kuachana na mwenza,kauli kama vile "Mimi nipo na mkosi,mimi nipo na laana,mimi nipo na nuksi,mimi sitakuja kupendwa ,hivi mimi ndiyo wa kupendwa na yule alinionea huruma tu."

c.Kujiapiza kutojihusisha na mapenzi maisha yao yote.atasema "sitakuja kuamini mtu yeyote hapa ulimwenguni maisha yangu yote - wanaume/wanawake wote ni mbwa"

d.Kujiepusha na mapenzi moja kwa moja kwa njia mbadala kama vile ulevi kupindukia, uvutaji bangi, kutumia dawa za kulevya,kujichua (masterbation),kufanya starehe sana,kutumia fedha nyingi sana ghafla,kufanya kazi muda wote,kula sana,kulala sana,kucheza video game, kuangalia video za ngono (pornography),wengine huamua kubadilisha wanawake au wanaume kila siku ili kuzuia kuja kupenda mtu yeyote mpaka mwisho wa maisha yao.

2. KUJITOA MHANGA KWA MWENZA WAKO SIYO GUARANTEE YA KUPENDWA WALA KUDUMU NAYE
Baada ya mahusiano kuvunjika ghafla ndipo utagundua kwamba kuhatarisha maisha yako,kujitesa,kujinyima chakula,kugombana na wazazi wako pamoja na ndugu zako, kumsomesha mwenza wako, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama kubwa sana,kumuuguza,kuwasomesha watoto wa mwenza wako, kuvumilia vipigo, matusi, unyanyasaji, udhalilishaji kutoka kwa mwenza wako,kuacha kazi kwa ajili ya kumfurahisha mwenza wako siyo GUARANTEE ya kupendwa wala kudumu naye.

Unaweza kujitoa mhanga kumfariji, kumlinda, kumliwaza, kumtetea, kubadilisha maisha ya mwenza wako kutoka kudhalilika mtaani mpaka kuheshimiwa mtaani kisha baada ya mwenza wako kufanikiwa anakuacha ghafla anakwenda kwa mtu mwingine bila kujali jasho lako na maumivu ambayo umepitia ili kumtetea pale ambapo alikuwa anapigwa vita na kila mtu.

Baada ya mahusiano kuvunjika ndiyo utagundua kwamba kujiwekea kauli kama "Niliwafanyia 1,2,3 wao pia wanatakiwa kunifanyia 1,2,3 nikiwa katika hali kama ya kwao" siyo utaratibu halisi katika maisha.

Siyo kila mtu anaweza kukupa kipaumbele katika maisha yake kama ambavyo wewe unaweza kumpa kipaumbele maishani mwako.

Maisha hayaendeshwi kwa tit for tat kwa kusema "Nimefanya 1,2,3 na wewe fanya 1,2,3 kama nilivyofanya kwako.
Kwenye Maisha halisi kila mtu yupo na utaratibu wake ambao kwake anaona ni sahihi.

Baada ya mahusiano kuvunjika ndipo utagundua kwamba kila mtu yupo hapa ulimwenguni kuandika historia yake na kila mtu atafanya makosa yake kivyake vyake na kila mtu atakuwa na njia zake za kukabiliana na matatizo yake.

Kila mtu atakuwa na njia zake za kuishi au kujifunza namna ya kuishi,kila mtu anawajibika kwa vitendo vyake na maamuzi yake.

Kila mtu yupo na uhuru wa kuchagua nini aamini na nini asiamini.
Unaweza kuwa na nia njema kwa mwenza wako lakini kwa sababu mwenza wako yupo na kumbukumbu mbaya juu ya njia ambayo unataka kuitumia lazima ataipinga hata kama kwako utaona ni njia sahihi.

3. KUACHA KUMTEGEMEA MWENZA WAKO KAMA CHANZO CHA FURAHA YAKO
Baada ya mahusiano kuvunjika ndipo utagundua kwamba mwenza wako hatakiwi kuwa chanzo cha furaha yako na endapo mwenza wako atakuwa chanzo pekee cha furaha yako utakuwa unalia kila siku.
Ukiwa hauna furaha utatamani kampani ya mwenza wako lakini yeye atakuona kero,atakuona mzigo,atakuona hauna pa kwenda.

Mwenza wako hawezi kukuthamini kama anakuona hauna furaha muda wote,ili mwenza wako awe na hofu ya kukupoteza anatakiwa akuone upo na furaha sana bila uwepo wake hapo atagundua kwamba endapo ataondoka hakuna pengo lolote ataliacha kwako.

Mtu yeyote unakuwa na hofu ya kumpoteza huwa ni yule ambaye unajua ukiondoka tu pengo lako linazibwa haraka na kumbukumbu zako zote anazisahau papohapo.

Kama mwenza wako anajua hauwezi kuwa na furaha maishani mwako endapo atakuacha utafanya mwenza wako awe na kiburi, majivuno, jeuri na dharau kwako kwa sababu atakuwa anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.

Lakini akiona upo na furaha sana pale ambapo anaondoka hofu ya kukuacha inazidi kuongezeka kwake siyo kwako.

4. HAUWEZI KUBADILISHA TABIA YA MWENZA WAKO IKIWA YEYE HAYUPO TAYARI KUBADILIKA
Haijalishi utakuwa ûnampenda sana mwenza wako lakini kitendo cha kutaka kumbadilisha tabia huwa ni kumkosea heshima.
je wewe unaweza kuruhusu mtu yeyote aje kukupangia namna ya kuendesha maisha yako?

utagundua kwamba mtu ambaye anataka kukubadilisha tabia huwa anageuka kero.
Binadamu kwa asili ni mbinafsi hivyo unapotaka abadilishe tabia anahisi ni kwa faida yako siyo yake.

Hakuna mtu ambaye anaweza kukubali akufurahishe wewe wakati yeye hana furaha labda kama atakuwa na tatizo.

Badala ya kutaka kumbadilisha tabia mwenza wako jiulize nini kimekuvutia kwake ?
mwanaume anavutiwa na Mwanamke mwenye tabia nzuri je wewe mwanaume unawezaje kuvutiwa kimapenzi na Mwanamke ambaye hana tabia njema ? ukiona unavutiwa kimapenzi na Mwanamke ambaye hana tabia njema ujue hauna sifa za mwanaume Rijali.

mwanaume Rijali huwa ni kiongozi mkuu wa familia kwa maana anatoa maagizo na sheria kisha Mwanamke anatii na endapo atagomea maagizo anaondoka.

Kwa upande wa Mwanamke sifa ya mwanaume ni uongozi hivyo kama mwanaume hawezi kukuongoza je umevutiwa na nini kwake ? ukiona unavutiwa kimapenzi na mwanaume ambaye hakutaki ujue hauna sifa za Mwanamke bali upo na hulka ya kiume.

Mwanamke mwenye hulka ya kiume huwa anataka kumpangia sheria mwanaume,huwa anataka kumtawala mwanaume,huwa anataka kubeba majukumu ya mwanaume.Ukiona unataka kumbadilisha tabia mwanaume ujue hauna role model mzuri kwanzia baba yako na kaka zako hakuna mwenye sifa za kiume bali huenda baba au kaka zako walikuwa na tabia za ubabe, ukatili, udikteta, udhalilishaji,hasira kupitiliza au walikuwa ni wanaume legelege ambao hawana uwezo wa kujiongoza.

Ukiona unamrekebisha mwanaume wako tabia ujue huyo mwanaume wako hajielewi wala hajui wajibu wake na vilevile wewe kama Mwanamke haujui mipaka yako ndiyo maana umegeuka mama mzazi kwa mwenza wako.

mwanaume simama sehemu yako vilevile Mwanamke simama sehemu yako hauwezi kuumizwa na mapenzi,ikiwa wewe mwanaume umeacha uanaume wako utasumbuliwa na mapenzi, vilevile Mwanamke ukiacha hulka yako ya kike na kuanza kuwa mwanaume ndani ya mwili wa Mwanamke utaona mwanaume anakuwa jeuri.

5. KUJIWEKEA MIPAKA HUSAIDIA KUBORESHA MAHUSIANO
Mwanaume ndiyo kiongozi katika familia,ikiwa mwanaume hawezi kumuonya mwanamke,hawezi kumpangia sheria,mwanaume hawezi kumuongoza mwanamke,mwanaume hawezi kumpa maagizo Mwanamke ujue kwamba huyo mwanaume hajui majukumu yake na vilevile Mwanamke hajui majukumu yake.

kama haujaweka mipaka katika mahusiano yako utaona mwenza wako anakula chochote,anavaa nguo yoyote,anakwenda kutembea mahali popote,anatumia fedha kiasi chochote bila kujali athari za kufanya hivyo.

mwenza wako akiona hauna mipaka ataanza kwa kuonyesha dharau,atakuwa jeuri,atakufokea, kukutukana, kukudhalilisha, kukujibu vibaya, kutishia muachane,, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano mara kwa mara atafanya haya kwa sababu anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.

mwanaume ndiyo anaonyesha njia ya mahusiano kupita siyo Mwanamke,ikiwa mwanaume hajielewi hapo Mwanamke atashika usukani lakini ugomvi na migogoro itaibuka mara kwa mara kwa sababu mwanaume huwa hakubali kuwa chini ya Mwanamke.

Mwanamke anapotaka kuwa kichwa huwa ni ishara ya dharau kwa mwanaume wake kwa sababu anakuwa anajiona mzuri sana,anajiona mwenye akili sana,anajiona mwerevu sana.

jambo la kuzingatia ni kwamba ikiwa mwanaume hawezi kumuongoza mwanamke kwenye njia sahihi Mwanamke atalazimika kusimama ngangari,atakuwa mbabe,atakuwa na misimamo mikali sana,atakuwa hataki kuambiwa makosa,atakuwa haambiliki, hashauriki, anakuwa na hasira kupitiliza hapo mahusiano kuvunjika ni rahisi.

Mwanamke akiwa mbabe anakuwa maalumu kwa ajili ya waume za watu pamoja na player ambao wanampa ujauzito na kumtelekeza.

mwanaume akiwa mstaarabu sana kuliko Mwanamke lazima ugomvi na migogoro itazidi kuongezeka kwa sababu sifa za upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu ni sifa za wife material sio sifa za mwanaume.

mwanaume Rijali sifa zake ni kiongozi mkuu wa familia,anatoa maagizo,anatoa onyo,anahakikisha usalama wa familia,anahakikisha chakula,nguo, matibabu na pesa za matumizi madogo madogo zinapatikana kwa wakati.

kisha tabia njema ya Mwanamke inalinda amani ya nyumba.
Ikiwa Mwanamke hana tabia njema basi ujue mwanaume yupo na tatizo.Ukiona mwanaume hajielewi vilevile Mwanamke hawezi kuishi kwa amani, utulivu na furaha kwa sababu furaha ya Mwanamke ipo kwenye uimara wa mwanaume.

Mwanaume dhaifu husababisha Mwanamke anateseka. 

Add Comments


EmoticonEmoticon